1.0 MAELEKEZO MUHIMU KWA WANAFUNZI WOTE WAOMBAJI MIKOPO
Waombaji mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2019/2020 wanakumbushwa yafuatayo:
(i) Kusoma na kufuata taratibu za maombi katika Mwongozo huu wa mwaka wa masomo
2019/2020;
(ii) Kuhakikisha kuwa maelezo unayoyatoa katika fomu ya maombi ya mkopo yawe sawa na maombi
ya udahili wa chuo. Unasisitizwa kuwa nambari ya mtihani wa kidato cha nne iwe sawa kwenye
maombi ya mkopo na udahili wa chuo.
(iii) Kuhakikisha kuwa nyaraka zote za maombi ya mkopo unazowasilisha ziwe zimehakikiwa na
mamlaka husika.
(iv) Kuhakikisha kwamba vyeti vyote vya kuzaliwa/vifo na vyeti vingine vinathibitishwa na mamlaka ya
vizazi na vifo (RITA) au Wakala watz
sajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar au Afisa aliyeteuliwa ili
kuthibitisha uhalali huo.
(v) Kuhakikisha vyeti vyote vya kuzaliwa/vifo kwa Wanafunzi waliozaliwa nchi za nje (wazazi waliofariki
nchi za nje) vithibitishwe na Balozi husika zilizopo ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
(vi) Waombaji wakamilishe fomu zao kwa usahihi na wakumbuke mara wanapowasilisha hawataweza
kurekebisha taarifa hizo iwapo hawakujaza kwa ufasaha.
(vii) Waombaji wote wanatakiwa kutunza nakala za maombi ya mkopo waliyowasilisha Bodi ya Mikopo
kwa matumizi mengine (kama itahitajika).
(viii) Waombaji wote wanakumbushwa kuzingatia muda wa mwisho wa kutuma maombi.
2.0 KWA UFUPI
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilianzishwa chini ya kifungu cha Sheria namba 9 ya
mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi Julai, 2005. Bodi ya Mikopo pamoja na majukumu mengine, ina
jukumu la kutoa mikopo au ruzuku kwa wanafunzi wenye sifa na wahitaji. Dirisha la uombaji mikopo
kwa mwaka wa masomo 2019/2020 litafunguliwa tarehe 01 Juni, 20199 na kufungwa tarehe 15
Agosti 2019.
3.0 USTAHIKI
Sheria na kanuni za Bodi ya Mikopo hutoa sifa na vigezo kwa ujumla kwa wanafunzi wahitaji wa
mikopo. Mwombaji stahiki na mhitaji anaweza kuomba mkopo /ruzuku ili kugharamia sehemu ya
gharama au gharama zote za masomo ya elimu ya juu.
3.1 UHITAJI
Mbali na sifa za jumla, vigezo vya ziada vinafafanua mwanafunzi mhitaji asizidi umri wa miaka
35 katika kipindi anachoomba mkopo, ambaye ni:
(i) Yatima (ambaye amepoteza wazazi wote wawili) au aliyepoteza mzazi mmoja, awasilishe
cheti cha kifo kilichothibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) au
‘Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar’
(ii) Mwombaji mwenye ulemavu uliothibitishwa na Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO), au
Wilaya (DMO), au chombo chochote kilichoidhinishwa kuthibitisha uhalali wa hali hiyo.
(iii) Mzazi mwenye ulemavu uliothibitishwa na Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO), au Wilaya
(DMO), au chombo chochote kilichoidhinishwa kuthibitisha uhalali wa hali hiyo.
(iv) Mwombaji anayetoka kwenye familia ya kipato cha chini au kaya maskini ambapo elimu
ya sekondari au Stashahada (diploma) alifadhiliwa na taasisi inayotambulika. Waombaji
wa aina hii wanatakiwa kutoa uthibitisho uliondikwa na taasisi hiyo kuthibitisha udhamini
huo.
(v) Mwombaji anayetoka kwenye familia ya kipato cha chini au kaya maskini anatakiwa
kuambatanisha namba ya TASAF ili kuthibitisha uhalali huo.
3.2 SIFA ZA JUMLA AMBAZO ZINATAMBULIKA KISHERIA
Vigezo vya jumla vinamtaka mwombaji mkopo atimize masharti yafuatayo: -
(i) Awe Mtanzania;
(ii) Awe ameomba mkopo kupitia mfumo wa maombi ya mkopo (OLAMS);
(iii) Awe amedahiliwa katika taasisi ya elimu ya juu inayotambulika, kwa muda wote,
isipokuwa wanafunzi waliodahiliwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (Open University of
Tanzania).
(iv) Asiwe na ufadhili mwingine
(v) Mwanafunzi anayeendelea na masomo mwenye matokeo/ripoti za matokeo zinazoonesha
ufaulu wa masomo yake ili kumwezesha kuendelea mwaka ujao au kwenda hatua
nyingine ya masomo.
(vi) Kwa mwanafunzi mnufaika ambaye anataka kuomba tena mkopo baada ya kusitisha
masomo/chuo anatakiwa alipe asilimia 25 ya fedha aliyoitumia kabla hajaomba mkopo
mpya, (malipo ya 25% ya mkopo wa awali siyo dhamana ya kupangiwa mkopo).
3.3 Vigezo na stahiki nyingine
(i) Mkopo utatolewa kwa kuangalia uhitaji na programu;
(ii) Waombaji wapya ambao kwa sasa wanaendelea na masomo, lazima wawe wamehitimu
elimu ya kidato cha sita (ACSEE) au stashahada (diploma) ndani ya miaka mitano,
kuanzia mwaka 2015 hadi 2019.
(iii) Waombaji wote waliodahiliwa kusoma shahada mbalimbali kwa mwaka wa masomo
2019/2020 wanapaswa wawe wamemaliza ACSEE/Stashahada au sifa nyingine
linganishi katika kipindi cha miaka mitatu, yaani 2017-2019.
4.0 MAKUNDI YA PROGRAMU
Baada ya kuainisha waombaji wahitaji, na kuonesha taratibu katika kipengele 3.1 na 3.2 hapo juu,
makundi ya programu zifuatazo zenye vipaumbele zitapewa mikopo kulingana na uwepo wa fedha.
4.1 KUNDI LA KWANZA
Kozi katika kundi la kwanza ni: -
(i) Ualimu wa Sayansi (Fizikia, Kemia na Baiolojia) na ualimu wa hisabati na masomo ya
biashara na Shahada ya uzamili katika Uhandisi wa Ndege na matengenezo
(ii) Sayansi za afya (Udaktari, upasuaji meno, madawa ya mifugo, Ufamasia, Uuguzi,
Ukunga, shahada ya sayansi katika Prosthetikia na Mifupa, Shahada ya sayansi katika
Mazoezi ya viungo, Shahada ya sayansi ya afya na maabara, Shahada ya sayansi ya
maabara na matibabu na shahada ya sayansi ya Teknolojia ya mionzi.
(iii) Programu za Uhandisi (Ujenzi, Mitambo, Umeme, Uchimbaji Madini,
Utengenezaji nguo, Kemikali na matayarisho, kilimo, Chakula na matayarisho,
Automobile, Viwanda, Umeme na elekroniki, Legal and Industrial Metrology, Usafiri
majini, Teknolojia ya uhandisi wa baharini, Elektronikia na mawasiliano, kompyuta,
programu za sayansi ya kompyuta, habari na mitandao, Mazingira, na Mipango miji,
usindikaji na huduma baada mavuno
(iv) Jiolojia ya petroli, kemia ya petroli
(v) Kilimo, Misitu, Sayansi ya wanyama na Usimamizi wa uzalishaji
4.2 KUNDI LA PILI
Kozi katika kundi hili ni:
(i) Programu za msingi za sayansi (shahada ya sayansi kwa ujumla katika wanyama,
mimea, kemia, fizikia, Baiolojia, baiolojia ya viumbe vidogo, baiolojia ya mifugo na
Bioteknolojia, Uvuvi na mifugo, Sayansi ya mazingira na uhifadhi, Matibabu, Hisabati na
takwimu, Sayansi ya mazingira na usimamizi, Afya na mazingira, Baioteknolojia na
maabara, Wanyamapori na uhifadhi, na Kompyuta); Tehama, vipimo na mizani, mazingira
na maendeleo ya miji.
(ii) Programu ya sayansi ya ardhi (Ubunifu majengo, Ubunifu mandhari nje ya majengo,
usanifu ndani ya majengo, Uchumi ujenzi, Mipango miji na vijiji, Usimamizi na uthaminishi
ardhi, Jiospasho, Teknolojia katika usanifu).
KUNDI LA TATU
Programu katika kundi hili ni pamoja na Biashara na Uongozi, Sayansi za jamii, Sanaa,
sheria, lugha, fasihi na masomo ya uandishi wa habari na mawasiliano. Programu
zingine zote ambazo hazijaorodheshwa katika makundi mengine zitaangukia katika
kundi hili la tatu. Shahada zingine zote ambazo hazikutajwa kwenye kundi la kwanza, la
pili au la tatu zitajumuishwa katika kundi la tatu.
5.0 VIPENGELE VYA MIKOPO, KING’AMUA UWEZO NA FEDHA INAYOPANGWA
Bodi ya mikopo inaweza kulipia gharama za baadhi au vipengele vyote hapo chini:
(i) Gharama za Chakula na Malazi
(ii) Ada ya Mafunzo
(iii) Vitabu na Viandikwa
(iv) Mahitaji Maalum ya Kitivo
(v) Utafiti
(vi) Mafunzo kwa Vitendo
5.1 Kipima/king’amua uwezo
Kipima uwezo kitatumika kuonesha uhitaji wa kifedha wa mwombaji. Malipo ya ada iliyolipwa
shule za sekondari (CSEE, ACSEE) pamoja na Stashahada (diploma) ni kigezo kimojawapo
kinachoangaliwa kubaini uwezo wa kuchangia gharama za elimu ya juu, vingine ni uyatima,
ulemavu, ufadhili na familia maskini.
Kwa maana hiyo, uhitaji utapimwa tofauti kati ya gharama za mwaka katika programu ya elimu
ya juu katika taasisi husika ya elimu ya juu dhidi ya gharama iliyotumika kulipia elimu ya
sekondari au stashahada (diploma) na uwezo wa mwombaji alioubainisha katika elimu ya
sekondari au diploma kama ishara ya uwezo wa mwombaji kuchangia gharama za elimu ya
juu.
5.2 MGAWANYO WA FEDHA KATIKA VIPENGELE VYA MKOPO
Upangaji mikopo kwa waombaji waliofanikiwa kupata mikopo utagawanywa kwa kuanza na
gharama za chakula na malazi, ikifuatiwa na Ada ya mafunzo, kisha vitabu na viandikwa
vikifuatiwa na mahitaji maalum ya kitivo, utafiti, na mwisho mafunzo kwa vitendo, kulingana
na kiasi kilichobakia kutoka vipengele vilivyotangulia.
5.3 Kiwango cha Ada ya mafunzo
Kiwango cha juu cha Ada kwa waombaji wote watakaofanikiwa kupata mikopo kitakuwa sawa
na gharama za ada zinazolipwa katika vyuo vikuu vya umma.
5.4 Mwanafunzi anayeendelea na masomo na ambaye ni mnufaika wa mkopo
Kwa wanafunzi wote wanufaika wanaoendelea na masomo wataendelea kupokea mikopo kama
awali kulingana na ufaulu wa mitihani yao. Wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao ni
wanufaika wa mikopo HAWARUHUSIWI KUOMBA MKOPO isipokuwa kwa wale wanafunzi
wahitaji ambao awali hawakupangiwa mikopo.
Utaratibu wa malipo: Gharama za chakula na malazi, vitabu na viandikwa, mafunzo kwa
vitendo, gharama za tafiti yatalipwa moja kwa moja kwa mwanafunzi wakati Ada ya mafunzo
na mahitaji maalum ya kitivo yatalipwa moja kwa moja kwenye taasisi husika ya elimu ya juu.
6.0 WAOMBAJI MIKOPO NJE YA NCHI (SHAHADA ZA KWANZA NA ZA UZAMILI)
Wanafunzi stahiki kwa mikopo kwa mwaka wa masomo 2019/2020 waliodahiliwa kusoma katika
vyuo vya nje ya nchi wanapaswa kutimiza masharti yaliyoorodheshwa katika Vigezo vya Jumla
Sehemu ya 2.1.
Pamoja na vigezo na masharti yaliyotajwa katika Sehemu ya 3.2, waombaji wa mikopo waliochaguliwa
na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pekee ndio watakaokuwa na sifa za kupatiwa mikopo ya
fedha za kujikimu isiyozidi USD 5400 kwa mwaka. Wanafunzi husika wanapaswa kuchaguliwa
kusoma nje ya nchi katika nchi ambazo zina makubaliano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.
7.0 MASHARTI MENGINE KATIKA UTOAJI MIKOPO
7.1 Wajibu wa mdhamini, wazazi na kamishna wa viapo
Wazazi/mdhamini wahakikishe usahihi wa taarifa zao ambazo zimewasilishwa katika fomu ya
maombi ya mkopo kabla ya kusainiwa. Wadhamini wanatakiwa kuhakikisha mikopo
inarejeshwa na lazima waelewe mahali wakopaji walipo walipe mikopo yao yote na ikitokea
hawajamaliza kulipa, mdhamini atalazimika kulipa mkopo huo.
Mdhamini anatakiwa kutumia nakala ya kopi ya kitambulisho mojawapo kati ya hizi ambayo
imethibitiswa
i. Kitambulisho cha Taifa
ii. Kadi ya mpiga kura
iii. Leseni ya udereva
iv. Pasi ya kusafiria
v. Kitambulisho cha Mzanzibari Mkazi
7.2 UREJESHAJI MIKOPO
Baada ya kuhitimu au kusitisha masomo ya elimu ya juu, mnufaika wa mkopo atatakiwa kurejesha
mkopo kwa makato si chini ya asilimia kumi na tano (15%) ya mshahatra wake wa kila mwezi. Mnufaika
ambaye amejiajiri anaweza kurejesha mkopo wake kwa kiwango kisichopungua shilingi laki moja
(100,000/=) kwa mwezi.
7.2.1 Mahitaji ya urejeshaji Mikopo
7.2.1.1 Tozo ya kulinda thamani ya fedha
Ili kuhakikisha mfuko wa ukopeshaji unakuwa endelevu, tozo ya kulinda
thamani ya fedha itakatwa asilimia sita (6%) kwa mwaka tangu tarehe
mnufaika aliyoanza kupokea mkopo.
7.2.1.2 Ada ya usajili
Bodi ya mikopo itakata asilimia moja (1%) ya ada ya usajili kwa mwanafunzi
mnufaika.
7.2.1.3 Ada ya makato ya adhabu
Ikiwa mnufaika atashindwa kulipa mkopo baada ya kipindi cha neema cha
miezi 24 baada ya kuhitimu masomo yake ataongezewa makato ya adhabu
ya asilimia kumi (10%).
8.0 KUHAMA CHUO AU PROGRAMU NDANI YA CHUO
HESLB haitafanya malipo ya mkopo kwa wanafunzi ambao watahama vyuo kwa hiari yao wenyewe.
Baada ya kupokea uthibitisho wa uhamisho wa chuo kutoka kwa mamlaka husika, uhamisho wa mkopo
utafanyika. Hakuna uhamisho wa mkopo utakaofanyika zaidi ya siku tisini (90) baada ya usajili.
Uhamisho wa mkopo utafanyika kulingana na kiasi cha mkopo kilichopangwa awali.
Orodha ya Waombaji waliopangiwa kwenye Taasisi za Elimu ya Juu
HESLB itazingatia maombi ya mkopo kutoka kwa wanafunzi waliodahiliwa katika Taasisi za Elimu ya
Juu na kuwasilishwa Bodi na mamlaka husika ikiwemo Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).
9.0 JINSI YA KUOMBA MKOPO
Maombi yote ya mkopo yatafanyika kupitia Mfumo wa Maombi na Usimamizi wa Mikopo (OLAMS).
Waombaji wote wa mikopo WANAKUMBUSHWA kutumia namba ileile ya Mtihani wa Kidato cha Nne
wakati wanapoomba vyuo.
Baada ya kukamilika kwa mchakato wa maombi kwenye mtandao, waombaji watapaswa kutoa nakala
za fomu za mombi na mikataba ya mkopo kwenye mtandao, kugonga mihuri sehemu husika, kusaini
fomu, kuambatanisha nyaraka zinazohitajika kwenye mtandao wa OLAMS kabla ya kutuma maombi
hayo kwa njia ya EMS kwa:
Mkurugenzi Mtendaji,
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
S.L.P 76068,
14113 Dar es Salaam, TANZANIA.
Waombaji wanakumbushwa kutunza nakala ya fomu za maombi, viambatanisho vilivyowasilishwa na
risiti ya EMS iliyotumiwa kutuma maombi yao kwa kufuatilia HESLB endapo itahitajika.
10.0 Ada ya Maombi ya Mkopo
Waombaji wanapaswa kulipia ada ya maombi ya mkopo ya kiasi cha shilingi elfu thelathini (30,000)
kupitia Benki ya NMB, CRDB au TPB.
Kwa maelezo zaidi tembelea: https:/olas.heslb.go.tz
Mwisho wa Kupokea Maombi
Dirisha la maombi ya Mkopo kwa mwaka 2019/2020 litafunguliwa kuanzia tarehe 15 Juni, 2019
hadi tarehe 15 Agosti, 2019.
Orodha ya Waombaji Watakaopangiwa Mikopo
Orodha ya waombaji watakaofanikiwa kupangiwa mikopo itatangazwa kwenye tovuti ya HESLB:
www.heslb.go.tz kabla au tarehe 25 Oktoba 2019.
11.0 Kukata Rufaa
Waombaji ambao hawataridhika na viwango vya mikopo watakayopangiwa wanaweza kukata rufaa
kwa kukamilisha fomu za rufaa kwenye mtandao (OLAMS). Maelezo zaidi yatatolewa baadaye.
12.0 Maulizo na Malalamiko
Waombaji au wanufaika wa mikopo wenye maswali au malalamiko watapaswa kufuata taratibu
zilizotolewa kwenye dirisha la maombi ya mkopo.
13.0 Wanafunzi wa Shahada za Uzamili na Uzamivu
Wanafunzi watakaokopeshwa kwa mwaka wa masomo 2019/2020, waliodahiliwa kujiunga na
Shahada za Uzamili na Uzamivu wanapaswa kuwa na sifa za jumla zilizoorodheshwa katika
kipengele cha 3.2 hapo juu.
13.1 Wanafunzi wa Uzamili na Uzamivu (Wahadhiri)
Mbali na sifa za jumla, waombaji wa Shahada za Uzamili na Uzamivu lazima wawe na vigezo maalum
vya kundi hilo, ambavyo ni:
(i) Wanapaswa wawe na Shahada ya Kwanza au Stashahada ya Juu na kiwango cha chini cha ufaulu kiwe
ni Daraja la Pili la Juu (Kwa waombaji wa Shahada ya Uzamili) au Shahada ya Uzamili na kiwango cha
chini cha ufaulu kiwe Daraja la Pili la Juu (Kwa waombaji wa Shahada ya Uzamivu).
(ii) Wanapaswa kuwa wahadhiri wa taasisi za elimu ya juu watakaodahiliwa kusoma masomo yao katika
taasisi za elimu ya juu zinazotambulika nchini Tanzania.
(iii) Wanapaswa kuteuliwa na kupatiwa kibali kutoka kwa mwajiri ambaye ni Mkuu wa Chuo wa taasisi
husika.
(iv) Wanapaswa kuwa wameanza kurejesha mikopo yao ya awali angalau kwa muda usiopungua miezi
kumi na miwili (12) au kurejesha kwa mkupuo mkopo stahiki kwa waombaji ambao awali walinufaika
na mikopo ya wanafunzi.
(v) Mwajiri lazima awe amesaini mkataba kati ya HESLB na taasisi husika ya elimu ya juu.
13.2 Wanafunzi wa shahada ya Uzamili na Uzamivu kwenye Taasisi ya Sayansi na Teknolojia
ya Nelson Mandela (NM-AIST)
Ili kuimarisha uwezo wa taifa katika utafiti, TEHAMA na uvumbuzi, HESLB inatoa mikopo kwa
wanafunzi waliodahiliwa kusoma Shahada za Uzamili na Uzamivu katika masomo yanayohusina
na Sayansi katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST).
Wanafunzi watakaokopeshwa kwa mwaka wa masomo 2019/2020, wanapaswa kuwa na sifa
za jumla zilizowekwa katika kipengele cha 3.2 hapo juu.
Mbali na sifa za jumla zilizowekwa katika kipengele 3.2 hapo juu, waombaji wa Uzamili NMAIST lazima watimize vigezo vingine maalum kwa Wanafunzi wa taasisi hiyo:
(i) Wawe wamedahiliwa katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NMAIST) katika shahada ya Uzamili au Shahada ya Uzamivu katika mojawapo ya kozi za
kipaumbele hapo chini:
• Sayansi ya Maisha
• Uhandisi wa Sayansi ya Hisabati na Kompyuta.
• Uhandisi wa Sayansi ya Habari na Mawasiliano.
• Sayansi ya Vifaa, Nishati, Maji na Mazingira.
(ii) Lazima wawe ni waajiriwa katika Taasisi za Umma na wawe wamefanya kazi kwa muda
usiopungua miaka miwili (2).
(iii) Lazima wawe wamedhaminiwa na waajiri wao kuhusiana na urejeshaji wa mikopo hiyo.
(iv) Lazima wawe wameanza kurejesha mikopo ya awali angalau kwa muda usiopungua miezi
kumi na mbili au kwa mkupuo kwa jumla ya miezi kumi na mbili kama hapo awali walikuwa
wanufaika wa mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.
(v) Marejesho ya mikopo ya wanafunzi wa Shahada ya Uzamili na Uzamivu wa NM-AIST
yataanza mara tu baada ya kumaliza mwaka wa kwanza wa masomo, kwa mwajiri
kuwasilisha Bodi ya Mikopo makato ya kila mwezi kutoka kwenye mshahara wa mnufaika.
13.3 Wanafunzi wa Shahada ya Uzamili waliodahiliwa katika Shule ya Sheria ya Tanzania
(LASCOT)
Wanafunzi wa Shule ya Sheria wanaostahili kukopeshwa kwa mwaka wa masomo 2019/2020
lazima wawe wametimiza masharti yafuatayo:
Lazima zawe na sifa za jumla zilizowekwa kipengele cha 3.2 hapo juu.
Mbali na sifa za jumla zilizowekwa kipengele cha 3.2 hapo juu, waombaji wa mikopo katika
Shule ya Sheria Tanzania (LASCOT) lazima wawe na vigezo maalum, ambavyo ni: -
(i) Wawe wamehitimu shahada ya sheria si zaidi ya miaka mitano nyuma (2014 to 2018);
(ii) Mikopo itatolewa kwa waombaji wahitaji tu kulingana na matokeo ya king’amua uwezo
wa mwombaji.
(iii) Ikiwa mwombaji ni mnufaika wa mkopo wa awali ambaye mkopo wake umekwishaiva,
anapaswa kuwa amerejesha kiasi chote kilichoiva kinachostahili kurejeshwa.
Mikopo ya Shule ya Sheria itatolewa kugharamia maeneo yafuatayo:
(i) Vitabu na gharama za viandikwa;
(ii) Ada ya mafunzo
13.4 Viwango vinavyotumika kwa Wanafunzi wa Shahada za Uzamili na Uzamivu
13.4.1 Chakula na Malazi
Bodi inatoa mikopo kwa ajili ya chakula na malazi kwa kiasi cha shilingi 10,000/=
kwa siku wakati wa mafunzo chuoni au wakati wa kukusanya data.
13.4.2 Gharama ya Vitabu na Viandikwa
Kiasi cha shilingi 500,000/= kwa mwaka kwa vitabu na viandikwa hutolewa kwa
wanafunzi wa Shahada ya Uzamivu. Kiasi cha shilingi 200,000/= kwa mwaka kwa ajili
ya vitabu hutolewa kwa wanafunzi waliodahiliwa katika Shule ya Sheria ya Tanzania.
13.4.3 Ada ya Mafunzo
HESLB inatoa mikopo ya ada ya mafunzo kwa asilimia mia moja (100%) kulingana
na kiwango cha ada cha Taasisi ya Elimu ya Juu husika.
13.4.4 Gharama za Utafiti
HESLB inatoa asilimia mia moja (100%) ya gharama za utafiti kulingana na viwango
vinavyotumika na Taasisi ya Elimu ya Juu husika ambavyo huweza kuidhinishwa mara
kwa mara. Viwango vinavyotumika ni kiasi cha shilingi milioni mbili (2,000,000/=)
kwa mwaka kwa Shahada ya Uzamili na shilingi milioni tano (5,000,000/=) kwa
mwaka kwa Shahada ya Uzamivu.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
4 Juni, 2019
0 Comments