MUHIMU KWA WALE WOTE WANAOHITAJI KUOMBA MIKOPO KUTOKA HESLB JUU YA UHAKIKI WA VYETI VYA KUZALIWA NA VIFO

🚩Rita imetoa mwongozo ufutao;
➡ Mwombaji anatakiwa kuwasilisha nakala ya cheti katika ofisi ya mkuu wa wilaya alikopata cheti cha kuzaliwa.
➡Waombaji wanaoishi nje ya WILAYA Waliopata CHETI cha kuzaliwa waingie katika mtandao kwa anuani: http://uhakiki.rita.go.tz/uhakiki ili kupata maelezo ya jinsi ya kutuma nakala ya cheti na risiti ya malipo.
➡Baada ya uhakiki cheti kilichohakikiwa kitatumwa kupitia anuani ya mwombaji katika mtandao.
🚩Ada ya uhakiki kwa kila cheti ni Tshs.3,000/=
➡ ILIPWE KUPITIA BENKI YA NMB KWENYE AKAUNTI YA ADMINISTRATOR GENERAL COLLECTION ACCOUNT Na. 20610009881 au BENKI YA CRDB KWENYE AKAUNTI YA ADMINISTRATOR GENERAL COLLECTION ACCOUNT Na. 0150339892600
NOTE
➡kila mwombaji awasilishe/atume kivuli cha cheti kinachosomeka vizuri kwa ajili ya uhakiki ikiambatana na nakala ya risiti ya malipo.
➡ Pia utaratibu uliotajwa hapo juu utatumika kwa ajili ya kuhakiki vyeti vya vifo vya wazazi.
👉🏼 Rita inapenda kuwasisitiza waombaji wote kufuata utaratibu ulioelekezwa hapo juu ili kuepuka usumbufu. Kwa maelezo zaidi piga simu namba *0800117482*
➡ Imetolewa na wakala wa usajili na udhamini(RITA)